Sheria ya uchunguzi katika internet na simu yatiwa saini.
27 Desemba 2007Matangazo
Berlin. Rais wa Ujerumani Horst Köhler ametia saini kuwa sheria taratibu mpya juu ya vipi maafisa wanaweza kufanya uchunguzi kupitia mawasiliano ya simu.
Msemaji wa rais amesema kuwa Köhler ametia saini muswada huo baada ya kuamua kuwa hakuna kitu katika sheria hiyo ambacho kinakwenda kinyume na katiba ya nchi hiyo. Sheria hiyo , ambayo inaanza kufanyakazi Januari mosi, itaruhusu wana usalama kuchunguza matumizi ya internet na simu na kuhifadhi takwimu zilizokusanywa kwa kipindi cha takriban miezi sita. Mashirika yanayowakilisha waandishi wa habari na wanasheria yamemtaka rais kutosaini muswada huo wa sheria. Makundi kadha pamoja na watu binafsi yamesema kuwa yatapinga sheria hiyo katika mahakama kuu ya katiba ya Ujerumani.