1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sheria zinazodhibiti Makanisa kujadiliwa nchini Kenya

Halima Gongo14 Juni 2023

Jopo kazi lililochaguliwa na Rais wa Kenya William Ruto kupitia upya sheria zinazodhiti makanisa limeanza vikao vya kukusanya maoni katika kaunti za pwani ya Kenya.

Kenia | Kirche in Nairobi
Picha: Donwilson Odhiambo/ZUMA Wire/IMAGO

Mawakili wa mhubiri Ezekiel Odero wamesusia kikao kilichofanyika huko kilifi kwa madai kuwa wanajopo waliwanyima nafasi ya kutoa maoni yao.

Wakati huo huo, idadi ya maiti zilizofukuliwa katika msitu wa Shakahola imefikia 303 baada ya miili 19 zaidi kufukuliwa siku ya Jumanne.

Jopokazi lilichoundwa na Rais William Ruto likiwa na jukumu la kupitia miongozo ya makanisa na sehemu za kuabudu liliandaa mkutano katika Ukumbi wa Jawabu kaunti ya Kilifi pwani ya Kenya kwa ajili ya kukusanya maoni kutoka kwa viongozi wa kidini na wananchi.

Soma pia: Waliokufa kwa kuacha kula Kenya wapindukia watu 300

Wakiongozwa na liyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Kitaifa la Makanisa nchini Kenya Mutava Musyimi ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa jopo kazi hilo, viongozi wa kidini kutoka Kilifi wameitaka serikali kubuni chombo maalum ambalo litapewa mamlaka ya kuadhibu makanisa ambayo yanakwenda kinyume na kanuni na vilevile kudhibiti makanisa hapa nchini. Hii hapa sauti ya Mutava Musyimi, mwenyekiti wa jopokazi hilo.

Wakati mkutano ukiendelea mawakili wa Mhubiri Ezekiel Odero walitoka nje ya kikao hicho cha mashauriano kwa hasira kwa kile walichokitaja kuwa ubaguzi.

Soma zaidi: Waliofukuliwa Shakahola wafikia 211

Wakizungumza baada ya kutoka nje wakili Danstan Omari alimshutumu mwenyekiti wa jopokazi hilo kupuuza kwa makusudi mikono yao iliyoinuliwa kila walipotaka kutoa maoni ya mteja wao ambaye ni Mhubiri Ezekiel Odero.Wakili huyo amedai kuwa atasitisha shughuli za jopokazi hilo mahakamani.

Polisi walaumiwa

Polisi wa Kenya wakishuhudia kufukuliwa kwa miili ya watu huko Shakahola, Kaunti ya Kilifi.Picha: Stringer/REUTERS

Kwenye kikao hicho,viongozi hao wa kidini waliwalaumu maafisa wa polisi kwa kupuuzilia mbali taarifa ambazo walipokokea awali kuhusiana na matendo ya Paul mackenzie.

Hii leo jopo hilo limeelekea katika kaunti za lamu na Tanariver ili kukusanya maoni zaidi kutoka kwa viongozi wa kidini na wakazi maeneo hayo.

Hata hivyo, jopokazi hilo limekumbana na vikwazo vya kisheria huku baadhi ya viongozi wakihoji uhalali wake wa kusimamia mapitio ya sheria za dini nchini.

Hadi kufikia sasa idadi ya miili iliyofukuliwa shakahola imeongezeka na kufikia 303. Hii ni baada ya miili 19 zaidi kufukuliwa jana.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW