WHO: Kipindupindu kiliongezeka mwaka 2022
25 Septemba 2023Matangazo
Shirika la WHO limesema jana Jumapili kwamba, visa 470,000 viliripotiwa mwaka wa 2022 ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na visa 220,000 vya mwaka uliopita.
Hata hivyo wataalam wa WHO wanaamini kuwa takwimu hizo bado hazijitoshelezi na katika makadirio ya awali, lilitabiri kuwepo wagonjwa milioni 1.3 hadi 4 na vifo va hadi watu 143,000 kila mwaka.
Afghanistan, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi, Nigeria, Somalia na Syria ziliathirika zaidi katika mwaka ulioshuhudia mlipuko wa juu zaidi ya ugonjwa huo.
Milipuko ya kipindupindu inahusishwa zaidi na uhaba wa maji ya kunywa mahitaji, umaskini na migogoro, na kadiri mlipuko unavyoongezeka, ndivyo inavyozidi kuwa ngumu kudhibitiwa