Shirika la Frontex lakiuka haki za binadamu eneo la Balkan?
8 Januari 2021DW ilifanya mahojiano na Ali al-Ebrihim raia wa Syria anayeishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Sombor, nchini Serbia karibu na mpaka wa Hungary. Al-Ebrahim amesema Septemba, alisafiri kwa basi na wakimbizi wenzake kwenye mji wa kaskazini wa Ugiriki wa Loannina na hapo waliingia kwenye mpaka na Albania bila kukutana na polisi wa Ugiriki.
Lakini amesema walinzi wa mipaka wa shirika la Frontex waliwazuwiya nchini Albania na kuwakabidhi mikononi mwa viongozi wa nchi hiyo kwenye mji wa mpakani wa Kakavia. Alipohojiwa ilikufahamu vipi alifahamu kuwa ni maafisa wa shirika la Frontex, al-Ebrahim alijibu :niliweza kutambua kutokana na baji waliokuwa wakivaa mikononi. Wafanya kazi wa shirika la usalama wa mipakani wa Umoja wa Ulaya,Frontex, wamevalia baji ya buluu ilionabendera ya EU.
Al-Ebrahim na wahamiaji wengine waliwaomba hifadhi viongozi wa Albania lakini waliambiwa kwamba haiwezekani kujaza fomu za kuomba hifadhi kutokana na janga la corona. Baadae walirejeshwa tena nchini Ugiriki, bila kuwataarifu kabla viongozi wa Ugiriki,alisema al-Ebrahim.
Al-Ebrahim alikuwa na bahati kwenye jaribio lake la pili. Alipanga kwenda Tirana,mji mkuu wa Albania na baadae Serbia kupitia Kosovo. Alisema alitaka kwenda Austria kupitia Hungary,lakini wasafirishaji haramu walimuomba euro 5,000 ilikumpeleka hadi karibu na mpaka wa Austria.
Frontex yakanusha tuhuma
Hope Barker, mratibu wa shirika la Wave-Thessaloniki,linalohusika na kuwahudumia kwa chakula,na huduma ya kiafya na ushauri wa kisheria wahamiaji wanaosafiri kwenye nchi za Balkan, amesema kwamba wanazo taarifa nyingi mfano wa hiyo ya al-Ebrahim kuhusu madhila ya wahamiaji na wakimbizi.
Barker ameiambia DW kwamba mji wa kaskazini wa Ugiriki ulikuwa eneo la hifadhi ya wahamiaji hadi hapo serikali ya chama kisichopenda mageuzi ilipoingia madarakani mwaka 2019.
Amesema hatua zisizo halali za kuwarejesha makwao wahamiaji , zinafanyika kwenye maeneo ya mpakani na hata ndani ya nchi. wahamiaji wanaojaribu kuingia kwenye nchi za Ulaya magharibi wanakwepa kuwa na mawasilano yoyote na viongozi wa Ugiriki.
Mashirika ya kuwahudumia wakimbizi yanasema kulikuwa na hatua nyingi ya kuwarejesha nyuma wakimbizi na wahamiajai kwenye mpaka kati ya Macedonia na Albania pia. Baker amesema kwamba mashahidi waliwasikia maafisa waliohusika na operesheni hizo wakizungumza kijerumani kwa mfano na wakiwa na baji ya buluu na yenye nembo ya Umoja wa Ulaya.
Shirika la Frontex limetupilia mbali madai hayo, msemaji wa shirika hilo ameiambia DW kwamba waliendesha uchunguzi na hawakupata ushahidi wa kutosha wa madai hayo.