Shirika la HRW: Askari wa Msumbiji wamewaua watoto 10
25 Novemba 2024Human Rights Watch imeongeza kuwa polisi imewakamata "mamia ya watoto bila ya kuzijulisha familia zao, hatua ambayo ni kinyume na sheria za kimataifa za haki za binadamu."
Hata hivyo, mamlaka haijajibu ripoti hiyo iliyotolewa na Human Rights Watch.
Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika imekumbwa na ghasia tangu uchaguzi wa Oktoba 9 ulioshindwa na chama tawala cha Frelimo ambacho kimekuwa madarakani tangu uhuru, ingawa matokeo hayo yamepingwa na upinzani.
Maelfu ya watu wameandamana kote nchini katika wiki za hivi karibuni, japo maandamano hayo yamekabiliwa vikali na polisi.
Rais Filipe Nyusi ambaye anatarajiwa kuondoka madarakani mnamo mwezi Januari, amelaani kile alichokiita "jaribio la kuchochea machafuko” katika hotuba ya hali ya taifa aliyoitoa wiki iliyopita.