Shirika la HRW laitaka Kenya kuacha kuwafukuza makambini waliochwa bila makaazi
23 Mei 2008Matangazo
NAIROBI
Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch limeitaka serikali ya Kenya kuacha kuwalazimisha kurudi makwao watu walioachwa bila makaazi kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi.Kwa mujibu wa mkurugenzi wa shirika hilo kanda ya Afrika Georgette Gagnon makambi ya wakimbizi wa ndani yamekuwa yakifungwa bila ya kutoleta notisi na pia mashirika yasiyo ya kiserikali yameshuhudia polisi wakiwatimua kwa nguvu watu walioko makambini katika eneo la Rift Valley,magharibi mwa Kenya ambako ghasia za uchaguzi zilisababisha athari kubwa.
Kiasi cha watu laki tatu na nusu walikimbia makaazi yao baada ya uchaguzi ambapo machafuko yaliibuka kufuatia mvutano kuhusu matokeo ya uchaguzi wa rais kati ya Raila Odinga na rais Mwai Kibaki.