1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Human Rights Watch yaishtumu RSF kwa dhulma za kingono Sudan

29 Julai 2024

Human Rights Watch imelishtumu kundi la wanamgambo wa RSF kwa vurugu za kingono dhidi ya wanawake ikiwemo ubakaji, ndoa za kulazimisha na kuozesha watoto. Matukio machache ya vurugu hizo yamehusishwa na jeshi la taifa.

Wakimbizi wa Sudan wakishuka kwenye lori lililokuwa limepakia familia zilizowasili katika kambi ya wakimbizi huko Renk, Februari 13, 2024.
Wakimbizi wa Sudan wakishuka kwenye lori lililokuwa limepakia familia zilizowasili katika kambi ya wakimbizi huko Renk, Februari 13, 2024.Picha: LUIS TATO/AFP

Human Rights Watch imeutaka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuunda tume ya pamona ya kulinda raia nchini Sudan, wakati ambapo vita vya zaidi ya miezi 15 kati ya jeshi la kundi la RSF havionyeshi dalili za kukoma.

Katika ripoti mpya yenye kichwa cha 'Khartoum Siyo Salama kwa Wanawake,' shirika hilo la kuteteta haki za binadamu limerikodi ushuhuda wa wafanyakazi 42 wa afya na watoa huduma ya kwanza kuhusu vurugu za kingono na ndoa za kulazimisha na za watoto, tangu kuzuka kwa vita Aprili 2023, kati ya Jeshi la Sudan na kundi la Rapid Support Forces, RSF.

Soma pia:  Marekani yaandaa mazungumzo ya kusitisha mapigano Sudan

Kati ya Aprili na Februari 2024, taasisi 18 huduma za afya ziliwatibu manusura 262 wa vurugu za kingono katika mkoa mkubwa wa Khartoum, ambao unajumlisha mji wa Omdruman ulioko mkabala wa Mto Nile.

Hata hivyo kulingana na watoa huduma ya kwanza, idadi ya visa vilivyoripotiwa ni sehemu ndogoi tu ya idadi halisi, huku manusura wengi zaidi wakikosa au kutokuwa tayari kutafuta huduma ya dharura.

Kikosi cha wanamgambo cha RSFPicha: Mohamed Babiker/Photoshot/picture alliance

RSF wamebaka, kubaka kimakundi na kuwalaazimish wanawake na wasichana wasiohesabika katika maeneo ya makaazi ya mji mkuu wa Sudan kuolewa, alisema Laetitia Bader, naibu mkurugenzi wa Human Rights Watch barani Afrika, na kuongeza kuwa kundi hilo limewaogofya wanawake na wasichana, na kwamba pande zote mbili zimekuwa zikiwazuwia waathirika kupata huduma za msaada, hali inayozidisha madhila wanayokabiliana nayo, na kuwafnaya wahisi kwamba hakuna mahala salama.

Tuhuma hizi za ubakaji zimetolewa pia na shirika la msaada la Madaktari wasio na Mipaka, MSF, ambalo katika ripoti yake ya tarehe 22 mwezi huu wa Julai lilizishtumu pande mbili zinazopigana kutothamini maisha ya binadamu na kutoheshimu sheria ya kimataifa.

Matukio ya ubakaji hayaripotiwi ipasavyo

Mkurugenzi Mkuu wa MSF Uholazi Vickie Hawkins, alisema matukio ya ubakaji na vurugu za kijinsia haviripotiwi ipasavyo kwa hofu ya waathirika kulipiziwa kisasi.

"Vurugu za kingono na kijinsia zimeenea pakubwa, lakini zinaripoti kidogo sana kutokana na hofu ya unyanyapaa, kunyamaza kwa hofu ya kulipiziwa kisasi na ukosefu wa huduma na nafasi za faragha. Data kutoka vituo vya MSF vinavyowasaidia wakimbizi wa Sudan nchini Chad zinaonyesha matumizi makubwa ya dhulma za kingono kama kipengee cha mzozo, hasa zikiwalenga wanawake na wasichana."

Zaidi ya watu 550,000 wamekimbia vita nchini Sudan na kuelekea Sudan Kusini tangu kuzuka kwa vita kati ya jeshi la Sudan na RSF Aprili 2023, kulingana na Umoja wa Mataifa.Picha: LUIS TATO/AFP

Ripoti ya Human Rights Watch yenye kurasa 88 pia inaainisha mazingira ambayo yanaweza kuhesabiwa kama utumwa wa kingono. Ingawa vurugu za kingono zimetambuliwa hasa kama silaha inyotumiwa na RSF, kumekuwaa na ripoti za vurugu za kingono zinazofanywa na wanajeshi wa serikali.

Soma pia: Daglo akaribisha mazungumzo ya kusitisha mapigano Sudan 

Human Rights Watch inasema kumekuwa na ongezeko la visa vilivyoripotiwa tangu jeshi lilipotwaa udhibiti wa mji wa Omdurman mapemwa mwaka 2024.

Kote nchini Sudan, manusura wameripoti majeraha mabaya ya kimwili kutokana na mashambulizi ya kingono, yakiwemo wanayofanyiwa na wapiganaji kadhaa mara moja. Miongoni mwa waliotibiwa na wahudumu wa afya ambao Human Rights Watch ilizungumza nao, wanawake wasiopungua wanne walifariki kutokana na majera yao.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW