Shirika la IAEA limeitaka Iran ''kushirikiana haraka''
9 Machi 2020Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya atomiki (IAEA) limeitaka Iran kushirikiana haraka
Kiongozi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya atomiki (IAEA) , Rafael Mariano Grossi,jumatatu ameiomba kwa mara nyingine tena Iran ''kushirikiana haraka na kikamilifu'' ilikuwaruhusu wachunguzi wake kutembelea maeneo mawili ambayo yanaaminika Iran ilirutubisha madini ya Uranium.
''Nimeitolea mwito Iran kushirikiana haraka na kikamilifu na shirika la IAEA,ikiwemo kuonyesha haraka maeneo muhimu'' alisema Grossi kiongozi mpya wa shirika hilo la umoja wa mataifa wakati wa ufunguzi mjini Vienna, wa mkutano wa baraza la magavana wa IAEA.
Iran yakeuka mkataba ?
Mwezi Januari, Iran ilikataa uchunguzi kwenye maeneo mawili ambayo shirika la IAEA lilitaka kuyafanyia uchunguzi. Maeneo hayo hayana uhusiano wa moja kwa moja na shruli za urutubishaji wa Uranium za hivi sasa,lakini yanahusika na miradi ya kinuklia kwa ajili ya matumizi ya kijeshi ya mwaka 2000.
'' Kukataa huko kunadhoohofisha uwezo wa shirika la IAEA wa kutoa taarifa za kuaminika za kutokueko na shughuli na vifaa vya kinukliya ambavyo havikutolewa ufafanuzi na serikali ya Iran'', aliongeza Grossi mbele wa wajumbe wa IAEA ambao wanashiriki kwenye mkutano wa kila baada ya miezi mitatu.
Utawala wa Iran umelezea kwamba haulazimiki tena kutoa taarifa kuhusu shuruli zake za kinuklia zilizofanyika kabla ya mkataba wa 2015,ambao hivi sasa uko kwenye kitisho cha kuvunjika.
Utawala wa Teheran umelilaumu shirika la IAEA kutowa taarifa hiyo kufuatia shinikizo la Israel na marekani.Kuangaziwa upya kwa mipango ya zamani ya kinyukliya ya Iran kunaweza kuzusha mivutano mepya.
Kuhusu mipango yake ya kisasa,Iran inaushirikiano wa wazi na wachunguzi wa shirika la umoja wa mataifa ambao wamepewa nafasi ya kutembelea maeneo yote muhimu.
Toka kujiondoa kwa Marekani kwenye mkataba kuhusu nukliya ya Iran mwaka 2018 na kuiwekea vikwazo nchi hiyo, Iran anajaribu kutoheshimu vipengee kadhaa vya mkataba huo ili kujikwamua kiuchumi.
Hatua ya hivi karibuni ya kutoheshimu mkataba huo, ni wakati Iran ilipotangaza tarehe 5 Januari kwamba itakiuka mkataba wa Nyuklia wa 2015 na kuvuka viwango vya urutubishaji madini ya Urani.