UchumiKenya
IMF yaidhinisha msaada wa dola milioni 600 kwa Kenya
31 Oktoba 2024Matangazo
Katika taarifa jana jioni, naibu wa kwanza wa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Gita Gopinath, alisema uchumi wa Kenya bado ni thabiti, huku ukuaji wake ukiwa zaidi ya wastani wa kikanda, kushuka kwa mfumuko wa bei, na kuongezeka kwa mapato kutoka nje yanayoisaidia sarafu ya nchi hiyo licha ya mazingira magumu ya kijamii na kiuchumi.
Hata hivyo, Gopinath amesema mapato na mauzo ya nje yamepungua hasa baada ya kufutiliwa mbali kwa muswada wa fedha.
Gopinath ameongeza kuwa mabadiliko magumu yako mbeleni na kwamba mazungumzo ya wazi kuhusu umuhimu na manufaa ya mabadiliko hayo ni muhimu.
Mkuu huyo wa IMF pia amesema msaada zaidi unahitajika kwa benki za Kenya pamoja na kushughulikia masuala ya utawala na ufisadi.