Shirika la INSO lakanusha madai ya upelelezi Burkina Faso
8 Oktoba 2025
Haya yanafanyika siku moja baada ya utawala wa kijeshi nchinihumo kusema limewakamata wafanyakazi wake.
Shirika la Kimataifa na Usalama, INSO, lililo na makao yake nchini Uholanzi limetoa tamko hilo kufuatia Waziri wa Usalama wa Burkina Faso, Mahamadou Sana kuwatuhumu wafanyakazi wao kwa "upelelezi na uhaini".
Katika taarifa, shirika hilo limesema linadhamiria kufanya kila liwezalo kuhakikisha wafanyakazi wake wanaachiwa. Mkurugenzi wa shirika hilo nchini Burkina Faso ni miongoni mwa wanaoshikiliwa.
Kwa upande wake Waziri Sana amesema wafanyakazi wa shirika hilo walichukua na kusambaza kwa mataifa ya kigeni, taarifa muhimu ambazo zingetishia usalama wa Burkina Faso.
Sana ameongeza kuwa shirika hilo lilipigwa marufuku kufanya kazi nchini humo mnamo Julai 31, ila baadhi ya wafanyakazi wake waliendelea na shughuli zao kwa siri.