1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSyria

Waasi nchini Syria wadhibiti eneo kubwa la Aleppo

30 Novemba 2024

Shirika linalofuatilia vita vya nchini Syria limesema katika ripoti yake ya leo Jumamosi, kwamba waasi nchini humo sasa wanadhibiti sehemu kubwa ya mji wa Aleppo.

Syria I Wapiganaji wa upinzani
Wapiganaji wa upinzani wa Syria wakiingia katika kijiji cha Anjara, magharibi mwa Aleppo, Syria, Novemba 28, 2024.Picha: Omar Albam/AP/picture alliance

Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu nchini Syria limesema makundi ya Hayat Tahrir al-Sham (HTS) na washirika wao yameteka sehemu kubwa za mji huo pamoja na vituo vya serikali na magereza.

Waasi hao wameendelea kushambulia vikosi vya serikali vinavyosaidiwa na Iran na Urusi tangu Jumatano, siku ambayo usitishaji vita ulianza rasmi nchini Lebanon kati ya Israel na Hezbollah inayoungwa mkono na Iran.

Urusi ilifanya mashambulizi ya angani usiku kwenye maeneo ya Aleppo kwa mara ya kwanza tangu 2016, na kufikisha idadi ya vifo 311,  vikiwemo vya wanajeshi 100, raia 28, na wanamgambo wa HTS na washirika wao 183.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW