Shirika la kutetea haki Tunisia lafungiwa kufanya kazi zake
25 Aprili 2026
Matangazo
Rais wa shirika hilo Bassem Trifi, amesema uamuzi huo umetolewa na mahakama ya mwanzo ya Tunisia na kwamba watakata rufaa. LTDH imeutaja uamuzi huo kuwa wa hatari, usiofuata haki wala misingi iliyo wazi.
Serikali yataja dosari za kiutawala
Shirika hilo limeelezwa kuwa shughuli zake zimesimamishwa kutokana na dosari za kiutawala, madai ambayo yameshawahi kutumika dhidi ya mashirika mengine yasiyo ya kiserikali. Tangu mwaka jana, zaidi ya mashirika 17 yamesimamishwa kwa muda nchini humo. Mashirika yakutetea haki za binadamu yamekuwa yakiikosoa serikali ya Rais Kais Saied kwa kukandamiza uhuru wa kiraia nchini humo.