Shirika la Msalaba Mwekundu latoa wito wa dharura Gaza
8 Januari 2025Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu limesema mvua kubwa na mafuriko yameharibu makazi ya muda huko Gaza, na na kufanya kufurika kwa maji hadi ya kina cha futi moja katika mahema yaliharibiwa vibaya.
Taarifa ilifafanua kuwa hali mbaya ya hewa ilikuwa "ikizidisha hali ngumu" huko Gaza, kwa kusema, kwamba familia nyingi ziliachwa bila hata mahitaji ya msingi, kama vile mablanketi. Ikinukuu Umoja wa Mataifa, taarifa hiyo iliangazia vifo vya watoto wanane wachanga waliokuwa wakiishi kwenye mahema bila vipasha joto au kinga yoyote kutokana na kunyesha kwa mvua na ongezeko la baridi.
Onyo la kutoka ndani katika eneo la Palestina
Inaelezwa kwamba Shirika la Hilali Nyekundi kwa Palestina linajitahidi kutoa huduma za afya za dharura na vifaa kwa watu wa Gaza, kwa nguvu za ziada na za uharaka katika kipindi hiki cha miezi ya baridi ya baridi. Lakini yameonya kuwa kukosekana kwa misaada na ufikiaji kunafanya kutoa msaada wa kutosha kuwa jambo lisilo wezekana.
Nalo Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) lilionya kuwa upatikanaji wa huduma za afya pia "umeathirika vibaya" katika sehemu za Ukingo wa Magharibi. Imesema inatokana na ongezeko kubwa la vikwazo vilivyowekwa na vikosi vya Israel tangu kuanza kwa vita huko Gaza. Shirika hilo ambalo limesema limehamua kusimamisha shughuli zake kwa muda wa miezi mitano kuanzia Desemba 2023, limevitaka vikosi vya Israel "kuacha kutekeleza hatua za vikwazo zinazozuia uwezo wa Wapalestina kupata huduma za kimsingi, ikiwa ni pamoja na matibabu".
Wafanyakazi wa misaada ya kiutu zaidi ya 300 wameuwawa
Kwa mujibu wa rekodi za Umoja wa Mataifa, zaidi ya wafanyakazi 330 wa kutoa huduma za kiutu wameuawa huko Gaza tangu Israel ianzishe vita vyake katika maeneo hayo katika kipindi kifupi baada ya shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023.
Na rekodi za hivi karibuni kutoka kwa wizara ya afya huko Gaza inayoeratibiwa na Hamas ni kwamba watu 51 wameuawa katika eneo la Palestina katika saa 24 zilizopita, na kufanya jumla ya vifo hadi wakati huu kufikia 45,936.
Soma zaidi:Watoto 7 wamekufa kwa baridi kali Gaza huku makumi wakiuawa
Wizara hiyo pia imesema katika taarifa yake kwamba takriban watu 109,274 wamejeruhiwa katika zaidi ya miezi 15 ya vita kati ya Israel na Hamas, vya tangu Oktoba 7, mwaka juzi.