Shirika la Ndege la Zimbabwe lanyang'anywa ndege
18 Mei 2011Matangazo
Kwa mujibu wa mkuu wa shirika hilo la Air Zimbabwe, Innocent Mavhunga, hatua hiyo imelifanya shirika lake kubakia na safari moja tu ya kutoka Harare kuelekea London, pamoja na safari nyingine mbili za ndani ya nchi.
Air Zimbabwe ilikuwa imekodi ndege aina ya Boeing 737-500 kutoka shirika moja la ndege la Zambia linaloitwa Zambezi, lakini sasa Zambezi limeichukua ndege yake.
Mgogoro huo umekuja siku chache baada ya shirika hilo la ndege la Zimbabwe kutimuliwa kutoka chama kinachohusika na safari za ndege za Kimataifa, IATA, kutokana na kudaiwa zaidi ya dola 280,000 za Kimarekani.
Mwandishi: Saumu Ramadhani Yusuf
Mhariri: Mohammed Khelef