1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirika la Oxfam laelezea mashaka ya hali ya kiutu Gaza

23 Desemba 2024

Shirika la misaada la Oxfam katika ripoti yake limesema ni malori 12 pekee yaliyosambaza chakula na maji katika eneo la kaskazini mwa Ukanda wa Gaza katika muda wa miezi miwili na nusu.

Gaza | Nachwirkung der israelischen Angriffe in Schule von Al-Ahli Arab
Wapalestina wakiwabeba watu waliojeruhiwa, baada shambulizi la Israeli shuleni katika Jiji la Gaza Desemba 19, 2024.Picha: Hadi Daoud/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Oxfam imesema hali hiyo inaibua wasiwasi juu ya hali mbaya ya kibinadamu katika eneo lililozingirwa la Palestina. Israel imeipinga ripoti hiyo, ikisema imetolewa makusudi na isivyo sahihi kwa nia ya kupuuza juhudi za serikali ya Israel za kufikisha misaada ya kibinadamu Gaza. Wizara ya afya katika Ukanda waGaza inayoendeshwa na Hamas imesema siku ya watu 58 wameuawa katika muda wa saa 24 zilizopita, na kufanya idadi ya vifo katika vita hivyo  kufikia watu 45,317. Wizara hiyo pia imesema kwamba watu zaidi ya laki moja na saba wamejeruhiwa katika vita vya zaidi ya miezi 14 kati ya Israel na kundi la Hamas, baada ya mashambulio yake ya Oktoba 7, mwaka 2023 katika ardhi ya Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW