1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Euro 2024 yatoa faida maradufu kwa shirika Deutsche Bahn

23 Juni 2024

Shirika la reli la Ujerumani linanufaika na maelfu ya mashabiki wa soka kutoka kote Ulaya ambao wamesafiri kuingia katika taifa hilo kwa ajili ya kutazama mechi za mchuano wa Euro 2024.

Euro 2024 Soka Serbia Uingereza
Mashabiki wa soka walipokusanyika kwenye stesheni ya treni kabla ya mechi ya Kundi C kati ya Serbia na Uingereza kwenye mashindano ya soka ya Euro 2024 mjini Gelsenkirchen, Ujerumani, Juni 16, 2024.Picha: Markus Schreiber/AP Photo/picture alliance

Mashabiki wa kandanda wakiwa katika treni wanaagiza vitafunwa na vinywaji kwenye treni wanapotoka mchezo mmoja hadi mwingine. Kwa mujibu wa taarifa ya juma la mwanzo ya mchuano huo ya kampuni ya reli Deutsche Bahn ni kwamba bia na soseji vinapungua sana.

Taarifa inasema mashabiki wenye kiu waliweza kunywa litna 44,588 za biakatiya Juni 14 na 19, ikiwa ni mara mbili ya mauzo ya kawaida ya bidhaa hizo katika mabehewa.

Kwa mujibu wa shirika  Deutsche Bahn zaidi ya mashabiki milioni 3 walisafiri kwenye treni za mwendo wa kasi za Ujerumani ile ya ICE kwa wakati huo, wakiambatana na wafanyikazi 150,000.