Shirika la misaada ya kiutu OCHA kupunguza wafanyakazi 2,600
12 Aprili 2025
Mkuu wa OCHA Tom Fletcher katika barua yake amesema bajeti ya OCHA inakaribia dola milioni 430 kwa mwaka lakini baadhi ya nchi zimepunguza michango yake kwa shirika hilo
Ameitolea mfano Marekani ambayo ni mfadhili mkubwa wa shirika hilo kuwa imeondoa mchango wake wa asilimia 20 sawa na dola za kimarekani milioni 63 iliyokuwa imetengewa mwaka huu wa 2025.
Soma zaidi: Mashirika yaunga mkono ombi la UN la dola bilioni 7
Fletcher, ameongeza kuwa kutokana na uhaba wa fedha unaolikabili shirika hilo, sasa linahitaji kubadilisha namna ya utendaji wa shuguli zake ili kuendana na rasilimali. Shirika hilo sasa litapunguza uwepo wake na kazi zake katika nchi za Cameroon, Colombia, Eritrea, Iraq, Libya, Nigeria, Pakistan, Zimbabwe na katika eneo la Gaziantep nchini Uturuki.