Shirika la Umoja wa Mataifa UNHCR, kuhusu swala la wakimbizi wa Somalia
9 Juni 2009Matangazo
Wakaazi hao Wanawake na wasichana wanabakwa na maeneo ya raia kushambuliwa kwa makombora, jambo ambalo limewalazimisha zaidi ya watu laki moja kuyakimbia majumba yao katika mwezi uliopita wa Mei peke yake. Fujo na mapigano yamesababisha mwezi uliopita kuuwawa watu wapatao 200.
Othman Miraji amezungumza na msemaji wa Shirika la UNHCR huko Nairobi, Emmanuel Nyabera kuhusu namna Kenya inavowapokea wakimbizi kutoka Somalia.
Mwandishi: Othman Miraji
Mhariri: Josephat Charo