1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNRWA yasitisha shughuli zake kufuatia wasiwasi wa usalama

1 Desemba 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Wakipalestina UNRWA,limesitisha shughuli zake za kupeleka msaada katika eneo la kivuko la Kerem Shalom lililoko kati ya Israel na Gaza kufuatia wasiwasi wa kiusalama.

Nahostkonflikt - UN-Hilfswerk für palästinensische Flüchtlinge
Lori la mizigo la Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina.Picha: Gehad Hamdy/picture alliance/dpa

Mkuu wa shirika hilo amesema barabara ya eneo hilo sio salama kwa kipindi cha miezi kadhaa sasa.  Phillipe Lazzarini amesema kupitia ujumbe alioandika kwenye ukurasa wake wa X kwamba msafara wa malori ya msaada ulivamiwa na kuporwa na magenge ya watu wenye silaha jana wakati wakijaribu kupeleka msaada kupitia njia hiyo. Mkuu huyo wa UNRWAameonya kwamba njaa inaongezeka katika ukanda wa Gaza. Ameitaka Israel kuhakikisha msaada unaingia katika Ukanda wa Gaza kwa kujizuia kushambulia wafanyakazi wa kutowa msaada wa kibinadamu. Jana shambulio la Israel liliwauwa wafanyakazi watatu wa shirika la msaada la Marekani la World Central Kitchen, akiwemo mmoja ambaye jeshi la Israel limesema alihusika kwenye uvamizi wa Oktoba 7, 2023 uliofanywa na Hamas.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW