Shirika la WFP larejesha msaada wa chakula Ethiopia
8 Agosti 2023Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP limeanza taratibu kurejesha shughuli za kupeleka misaada ya chakula nchini Ethiopia karibu miezi mitano baada ya kusitisha huduma hizo. WFP ilichukua hatua hiyo isiyo za kawaida baada ya kugundua mpango wake unafanyiwa hujuma za kuiba nafaka kwa ajili ya misaada.
Shirika hilo limesema linajaribu kusambaza misaada kwa uchache katika baadhi ya maeneo nalimesisitiza kwamba serikali bado ina jukumu katika mchakato huo.
Wakosoaji ikiwemo mashirika ya misaada na wafanyikazi wa afya, walilaani kusitishwa kwa misaada hatua ambayo walisema ni kinyume cha maadili. Wamesema mamia ya watu walikufa kwa njaa. Marekani, hata hivyo imesema itaendelea kusitisha msaada wa chakula wakati ikijadiliana na serikali ya Ethiopia kwa ajili ya mageuzi ya mfumo unaodhibitiwa kwa muda mrefu na mamlaka za ndani.