Shirikisho la Afrika Mashariki litaahirishwa kuundwa
21 Agosti 2007
Marais wa nchi tano za jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubaliana kuahirisha uundwaji wa shirikisho la Afrika Mashariki ifikapo mwaka 2013, ili kutoa nafasi kwa nchi za Rwanda na Burundi kukusanya maoni ya wananchi wake iwapo wanakubaliana na hatua hiyo.
Matangazo
Rwanda na Burundi ni wanachama wapya wa jumuiya hiyo. Marais hao walikubaliana hayo katika mkutano wao uliyofanyika huko Arusha nchini Tanzania.
Kutoka Arusha mwandishi wetu Charles Ngereza anaripoti zaidi.