Shirikisho la Riadha Duniani latoa mapendekezo
24 Januari 2023Matangazo
Pendekezo hilo linachukua mtizamo tofauti na michezo mingine ambayo imepiga marufuku wanamichezo waliobadili jinsia kushiriki katika mashindano ya wanawake.
Waraka unaoonyesha sera ya shirikisho hilo la riadha umewasilishwa kwa mashirikisho ya kitaifa wanachama katika mchakato wa mashauriano kabla ya kupigiwa kura mwezi Machi.
Katika taarifa, Shirikisho la Riadha Ulimwenguni limesema chaguo lake linalopendelewa ni kuimarisha sheria zinazohusu ustahiki lakini kwamba linataka kutumia ukomo wa homoni za kiume za testosterone kama kigezo muhimu cha kuzingatiwa.
Michezo mingine kama vile kuogelea imewapiga marufuku wanawake waliobadili jinsia kushiriki katika mashindano kwa sababu ya wasiwasi kuwa wana faida isiyo ya haki.