SiasaMisri
Shoigu awasili Misri kwa mazungumzo ya kijeshi
10 Novemba 2025
Matangazo
Shoigu aliyewasili siku ya Jumapili (Novemba 10) alitarajiwa kukutana na Rais Abdel Fattal al-Sisi, mshauri mkuu wa usalama wa Misri, mawaziri wa nje na ulinzi, na pia maafisa wengine wa ngazi za juu wa ulinzi na ujasusi.
Shirika la habari la Urusi, RIA, liliinukuu taarifa kutoka Baraza la Usalama la nchi hiyo ikisema kwamba pande hizo mbili zingelijadiliana utekelezaji wa makubaliano yaliyokwishafikiwa katika ngazi za juu, ukiwemo ushirikiano wa kiufundi kwenye masuala ya kijeshi.
Shoigu, mshirika wa muda mrefu wa Rais Vladimir Putin wa Urusi na waziri wake wa zamani wa ulinzi, anaendelea kuwa mtu mwenye nguvu sana kwenye mfumo wa kijeshi wa Kremlin.