Shughuli za hatari za kampuni ya Blackwater.
26 Februari 2008Matangazo
Kampuni ya ulinzi Blackwater ya Marekani ambayo imeajiriwa na utawala Bush kulinda usalama nchini Irak, mwaka jana ilihusika na mauaji ya raia 17 mjini Baghdad.
Pia pana madai kwamba kampuni hiyo inajihusisha na biashara ya silaha.
Raia hao walidaiwa kuwa na nia ya kuwashambulia wamarekani.
Wairaki wengine 24 walijeruhiwa katika shambulio hilo.
Lakini tofauti na mikasa mingi mingine, tukio hilo lilizingatiwa kwenye bunge la Marekani lakini hakuna hatua yoyote thabiti iliyochukuliwa dhidi ya kampuni hiyo ya Blackwater.
Mwandishi na mchapishaji wa Marekani Jeremy Scahill amendika kitabu juu ya shughuli za kampuni hizo ambazo ameziita kuwa ni majeshi ya watu binafsi.