1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaUturuki

Shughuli za uokoaji zaendelea Uturuki na Syria

11 Februari 2023

Shughuli za uokoaji nchini Uturuki na Syria zimeendelea leo Jumamosi, ikiwa ni siku tano baada ya kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi ambalo hadi sasa limegharimu maisha ya watu zaidi ya 24,000.

Türkei | Erdbeben | Suche nach Verschütteten in Adana
Picha: Teri Schultz/DW

Zaidi ya vikosi 166,000 vya uokoaji wakiwemo wasaidizi 8000 wa kigeni wameendelea na juhudi za kuwasaka manusura wa janga hilo la asili. Licha ya kufifia kwa matumaini ya kuokoa watu zaidi, bado watu kadhaa wamekuwa wakiokolewa wakiwa hai kutoka chini ya vifusi.

Serikali ya Bangladesh imetuma misaada ya kibinaadamu pamoja na madawa kwa waathiriwa huko Syriahuku ikituma katika nchi hizo mbili timu ya waokoaji. Hata hivyo hali ya hewa ya baridi kali imesababisha ugumu wa maisha kwa wale walionusurika na hata vikosi vya waokoaji.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW