Sierra Leone yatangaza hali ya dharura ya Mpox
14 Januari 2025Wizara ya afya nchini humo imesema hakuna mgonjwa yoyote kati ya hao wawili waliokutwa na Mpox aliyekaribiana hivi karibuni na wagonjwa wengine.
Inaripotiwa kwamba mgonjwa mmoja, alisafiri hivi karibuni katika mji wa Lungi ulioko wilaya ya Port Loko kaskazini kati ya Disemba 26 na Januari 6.
Wagonjwa wote wawili wanapokea matibabu katika hospitali ya mji mkuu Freetown.
Soma pia: Ugonjwa wa Mpox wazidi kuenea Burundi
Sierra Leone ilikuwa kuwa kitovu cha mlipuko wa ugonjwa wa Ebola mnamo mwaka 2014, mlipuko mbaya zaidi katika historia.
Mlipuko huo, ulioenea zaidi eneo la Afrika Magharibi, uliiathiri zaidi Sierra Leone huku vifo vya karibu watu 4,000 vikiripotiwa nchini humo kati ya vifo 11,000 vilivyorekodiwa duniani kote.
Nchi hiyo pia ilipoteza asilimia saba ya wafanyikazi wake wa kutoa huduma ya afya kutokana na mlipuko huo wa Ebola.