1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sigmar Gabriel ajitoa kushiriki serikali mpya

Sekione Kitojo
8 Machi 2018

Sigmar Gabriel mwenye umri wa miaka 58, wa chama cha SPD, ameamua hatojumuika katika serikali mpya ya muungano na vyama vya kihafidhina vinavyoongozwa na Kansela Angela Merkel katika serikali ya muungano mkuu GroKo.

Sigmar Gabriel SPD Parteitag
Picha: picture-alliance/AP/M. Schreiber

Siku  ya Alhamis Gabriel alitumia mtandao  wa  kijamii  wa  Twitter  kutuma  ujumbe  wake kwa umma kwamba  hatokuwa mmoja  wa  wajumbe wa SPD katika  serikali mpya ya Ujerumani.

Ametaka  chama  chake, mbali ya  kuwa  aliwahi  kuwa  mwenyekiti  wa chama  hicho  cha  SPD, kukifahamisha  wazi. Kwasababu  uongozi mpya  wa  Olaf Scholz  na mwenyekiti  mtarajiwa  Andrea Nahles unataka  hadi  ifikapo  kesho  Ijumaa  asubuhi  kutangaza, nani watakuwamo  katika  baraza  la  mawaziri  la kansela  Angela  Merkel. Na  nani  anaondoka. Lakini  kuhusiana  na  mipango  ya  Sigmar Gabriel,ameamua hatahusika.  Na  amekwisha  amua.

Sigmar Gabriel akiwa katika safari zake za kidiplomasiaPicha: picture-alliance/dpa/S.Stein

Kwa  hivi  sasa Gabriel  ndie  mwanasiasa  anayependwa  sana. Amefanikisha  kuachiwa  huru  kwa  mwandishi  habari   raia  wa Ujerumani  mwenye asili  ya  Uturuki  Deniz Yücel kupitia  diplomasia makini. Kutokana  na  hatua  za  uwazi  alizozichukua  kufanikisha  jambo hilo  hakuna mtu  atakayemsahau. Hakutafuna  maneno inapokuja  suala la  Donald Trump.

Anafanya  ziara  huku  na  huko  bila  kuchoka, kwenda  Moscow, na hadi  katika  mataifa  ya  eneo  la  Balkan. Na kwa muda  mfupi  kabisa  ameweza kupambana  na  wanachama  muhimu wa  chama  hicho. Kwanza  alimfanya  Martin Schulz  kuwa  mwenyekiti wa  chama  na  mgombea  wa  kiti cha ukansela, na  kuchafua  kampeni za uchaguzi. Kwanini ?  kama  kuna  mtu  anayefahamu.

Bado gharama zaidi zinawezekana ?  Mara  Gabriel  huwa mtetezi  wa sera  za  kiliberali  za  wakimbizi  za  kansela  na  kubandika  kabisa kauli  mbiu  ya  wakimbizi  mnakaribishwa  wakati  wa kikao  cha  bunge la  Ujerumani Bundestag, na  kisha  anaonya  dhidi  ya  kuwakandamiza Wajerumani  kuhusiana  na  kipato  chao  kidogo kwa  kuruhusu wahamiaji  wengi.

Baada ya  kushindwa uchaguzi  

Amesafiri  kwenda  Cairo  na  kukosoa  wakati  akiwa bado  katika  ndege  kukamatwa  watu  wengi  na  utawala  wa  Abdel Fattah  el-Sisi, na  kisha  kusema  mbele  ya  waandishi  habari kwamba  amefurahishwa  na  rais  huyo. Unaweza  kuzunguka  katika, duara  bila  kuonesha mwelekeo halisi, na  kuacha  mawazo  yako yakielea.

Martin Schulz aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha SPD na mgombea wa kiti cha ukanselaPicha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Baada  ya  kushindwa  vibaya  chama  chake  katika  uchaguzi  wa mwezi  Septemba  mwaka  jana alikishambulia  chama  chake  cha Social Democratic , kwa  kuchagua  watu  ambao  sio  sahihi, na kukumbatia misimamo  ambayo  si  sahihi. Kwa neno  moja: Kuwashawishi  zaidi  wale  wote  ambao  hawaridhishwi  kama  vile kuwawekea  mazingira  mazuri  ya watu  kupata  mishahara  bora  ama matibabu mazuri nchini.

Na tusisahau  kwamba , alikuwa  mkuu  wa  chama  hicho  kwa  muda wa  miaka  minane, muda  mrefu  zaidi  kuliko  mwenyekiti  yeyote mwingine  wa  chama  hicho baada  ya  Willy Brandt.

Ni  mtu  ambaye anaweza  kuwa  wa  utata, kwa  mambo  yake. Anachanganya  mambo  ya  kisiasa  na  ya  binafsi, anamuingiza  mtoto wake  wa  kike  katika  masuala  ya  umma, wakati  alipomwambia , anapaswa  sasa  kutumia  muda  wake  mwingi  zaidi  kwa mwanae  na asimwache  pamoja  na  yule  mtu  mwenye  madevu. Alikuwa  na maana  ya  Martin Schulz.

Maneno  ya kejeli  kabisa. Gabriel anaomba radhi , kila  mara. Anabahati  mbaya ,  kama  ilivyo  hivi  sasa  kwamba Andrea  nahles  ndie  mkuu  wa  chama  hicho, ambaye  alikuwa  katibu mkuu  wa  chama  chini  ya  uongozi  wa  Gabriel  kipindi  ambacho alifanyakazi  kwa  nguvu  zote. Mara  nyingi  alifanya  aonekane  kama mwanafunzi  msichana. Kwa  kuwa  gabriel  hakuweza  kumvumilia karibu akiwa  karibu  yake,  na  hakuwahi  kumuona  kama  kiongozi anayelingana  nae.

Mwandishi: Thurau, Jens / ZR/ Sekione  Kitojo

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW