1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya Afya Duniani

7 Aprili 2026

Siku ya afya Ulimwenguni. Na nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, vituo vingi vya afya vinakabiliwa na changamoto za upatikanaji wa dawa katika maeneo yenye vita, mashariki mwa nchi hiyo.

Indien Hyderabad 2013 | Vorbereitung einer Anti-Tabak-Kampagne im Apollo Cancer Hospital
Siku ya Afya duniani: Kauli mbinu mwaka 2026, Pamoja katika Afya, simama na sayansiPicha: Noah Seelam/AFP

Hali ya upatikanaji wa huduma za afya, ambayo tayari ilikuwa tete katika nyakati za kawaida, imezidi kuwa mbaya kutokana na miongo kadhaa ya migogoro ya kivita ambayo imevuruga sana mfumo wa huduma za hali hiyo inaongeza uwezekano wa raia kuathirika zaidi.

Wakazi wa vijiji mbalimbali wanalalamika kwamba ukosefu wa usalama unakwamisha utoaji wa dawa na vifaa tiba. Kwasasa, barabara nyingi zilizotumiwa kupeleka dawa vijijini hazipitiki na zingine zinadhibitiwa na watu wenye silaha, hali inayoongeza ugumu wa kusambaza dawa katika vituo vya afya kwenye maeneo ya vijijini. Godelive, mkazi wa kijiji cha Kabare anatoa malalamiko kwamba vita vimesababisha umaskini unaokwamisha wengi wasiweze kufikia huduma za matibabu, anaelezea pia changamoto zingine:

Miongoni mwa matokeo ya vurugu za kutumia silaha ni uharibifu wa miundombinu ya afya. Hospitali na zahanati nyingi zimeporwa, kuchomwa moto, au kuachwa bila wauguzi na madaktari ambao wamelazimika kukimbia kutokana na ukosefu wa usalama. Katika baadhi ya maeneo ya vijiji vya Kivu Kusini, wakazi wanalazimika kusafiri mwendo mrefu hadi kuvifikia vituo vya afya ambavyo bado vinafanya kazi, mara nyingi chini ya vitisho kutoka kwa makundi yenye silaha, Huduma zinazotolewa kwa wagonjwa kwenye vituo hivyo zimepunguza ubora.

Lakini pia, baadhi ya wakazi wanatoa malalamiko kuhusu Gharama ya huduma za afya kwa sababu ya kukosekana kwa mfumo madhubuti wa bima ya afya. Katika muktadha wa umaskini unaochochewa na idadi kubwa ya watu kuhama makazi yao kutokana na migogoro, familia nyingi zinakimbilia tiba za kitamaduni ambazo wakati mwingine zinahatarisha maisha yao.

Mwanaharakati wa Shirika la raia wa wilaya ya Mwenga, Mukambilwa Silibo anaeleza masikitiko kwamba Magonjwa yanayoweza kuzuilika yanaendelea kuathiri maisha ya wakazi kwa sababu ya kukosa dawa :

Katika eneo hili lenye vita, Daktari Baraka Musombwa Joseph anakumbusha kwamba waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono uliotumiwa sana kama silaha ya vita wanahitaji usaidizi wa kimatibabu na kisaikolojia:

Kwa miongo kadhaa, mashirika kadhaa ya kibinadamu yamekuwa yakijaribu kutoa majibu na kusaidia vituo vya afya ila kutokana na ukosefu wa usalama mashirika mengi yamehama maeneo na mengine sasa yanakabiliwa na upungufu wa fedha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW