1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya kimataifa ya wazee yaadhimishwa Oktoba mosi

1 Oktoba 2018

Kila tarehe mosi Oktoba dunia huungana pamoja kuadhimisha siku ya Kimataifa ya wazee duniani. Kauli mbiu ya mwaka huu 2018 ni kuwaenzi wazee watetezi wa haki za binaadamu.

Kenia Joyce Gichuna aus Nairobi
Picha: DW/R. Kyama

Takriban watu milioni 700 kwa sasa wamepindukia  umri wa miaka 60, na ifikapo mwaka 2050 watu bilioni 2 ambayo ni zaidi ya asilimia 20 ya idadi jumla ya watu duniani watafikisha umri wa miaka 60 au zaidi.

Kuongezeka kwa idadi ya wazee duniani litakuwa jambo kubwa na litakalokwenda haraka zaidi katika dunia ya sasa inayoendelea huku bara Asia likiwa na idadi kubwa ya wazee na Afrika nayo ikifuata kuwa na idadi hiyo kubwa ya wazee.

Bibi Mkongwe akifanya biashara yake katika barabara za IndiaPicha: DW/P. Tiwari

Kwa kuzingatia hayo wazee wanamahitaji makubwa na kuzeeka au kuwa mkongwe hakuondowi  utu na haki za msingi za mwanadamu, kama inavyosema ripoti ya Umoja wa Mataifa juu ya kuadhimisha siku hii ya Kimataifa ya wazee duniani.

Miaka 40 tangu kutangazwa kwa azimio la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 1991.

Umoja huo ulianzisha siku hii ya kuwaadhimisha wazee, kwa lengo la kutoa ulinzi kwenye masuala ya uhuru, ushiriki, huduma, heshima na utu wao. Umoja wa Mataifa unasema ni jukumu la vizazi vyote kulinda haki ya jamii inayozeeka.

Kila mkongwe anahitaji heshima na kutambuliwa katika mchango wake za kuchagia kupatikana kwa mabadiliko kwa vizazi vyao.

Kauli mbiu ya mwaka huu katika kuadhimisha siku ya wazee duniani ni kuwaenzi watetezi wazee wa haki za binaadamu, kwa kuimarisha haki zao, kuzidisha utambuzi wao katika jamii, na kutatua changamoto wanazopitia

Watetezi wazee waliopo leo walizaliwa mwaka 1948 ambao ni mwaka ambapo kwa mara ya kwanza tangazo la kuadhimisha haki za binaadamu (UDHR) lilitolewa.

Juma Ligaga mkongwe wa miaka 83 nchini TanzaniaPicha: DW/E. Boniphace

Wazee hao wapo tofauti kama ilivyo jamii wanamoishi kutoka kwa wazee wanaotetea haki zao za binaadamu katika kiwango cha chini na wale walio katika kiwango cha kimataifa.

Kila mmoja wa wazee hawa anahitaji heshima na kutambuliwa katika mchango wake na juhudi zake za kuchagia kupatikana kwa mabadiliko kwa vizazi vyao.

Kuanzishwa kwa siku hii kulifuatiwa na kile kinachotambuliwa kama Mpango wa Mkakati wa Madrid kwa Wazee (MIPAA) uliopitishwa mwaka 2002 na ambao ulizifanya serikali za mataifa wanachama kwa mara ya kwanza kuhusisha masuala ya uzee na mifumo mingine ya haki za kibinaadamu na maendeleo ya kiuchumi katika sera zao.

Mwandishi Amina Abubakar/UN Page

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW