Siku ya kulinda mbuga Ulaya
24 Mei 2017Leo ni sherehe ya kuadhimisha hifadhi ya maeneo asili ya mazingira nchini Ujerumani. Kuadhimisha siku hii Rais wa Shirikisho la hifadhi maeneno asilia ya mazingira ( BfN ) Prof. Beate Jessel, amesema kuwa Ujerumani ina sehemu kubwa ya maeneo ya asilia na maeneo hayo nimazuri, ya kuvutia na yenye thamani kubwa. Jessel alisema pia maeneo hayo makubwa ni sehemu ya urithi wa asilia yenye vitu vingi vya kujivunia vikiwemo mbuga za asili utajiri wa mauwa tafauti na milima mbalimbali. leo pia pia inaadhimisha siku ya mbuga, Ulaya nzima.
Siku hii ya "Siku ya mbuga" ilianzishwa tarehe 24 mwezi wa tano 1909. Wakati huo Mbuga ya mwanzo kuteuliwa na kupewa hifadhi ilikuwa bustani ya taifa nchini Sweden
Wasimamizi wanaoshirikiana na Ujerumani katika kutunza bustani na mazingira ya asilia ni shirika la EUROPARC. Hili ni Shirika ambalo ni mwamvuli unaozishirikisha nchi mbalimbali kutoka ulaya katika shughuli za kulinda maeneo asilia ya mazingira. Sehemu hizo nyingi za asili ziko nchini Ujerumani.
Nimezungumza na Jann Wilderfelt ambaye ni mwakilishi wa shirika la EUROPARC katika ofisi yao ya Berlin na nilimuuliza nini umuhimu wa siku kama hii ya leo kwa Ujerumani na Ulaya, alisema:
"Siku ya mbuga au bustani ni siku ya kuendeleza mokakati ya kuifadhi na kulinda maeneo asili ya mazingira. Na siku hii ni muhimu hapa Ujerumani na barani ulaya, kwa vile katika kulinda maeneo haya pia tunalinda pia rasili mali zetu za asili na menendo ya maisha yetu. Na watu wengi hawajui hilo. katika sehemu kubwa inayohifadhiwa barani ulaya kunahifadhiwa pia utaratibu asilia wa ukuaji na hifadhi ya mimea."
Prof. Beate Jesse amesema katika hotba yake kuwa Wajerumaniwengi wengependa kuwa na mbuga nyingi zaidi kuliko sasa. Kwahivyo alikaribisha mpango mpya wa jimbo la Bavaria wa kufungua hifadhi mpya ya tatu katika sehemu zilizo wazi.
Wilderfelt anaelezea zaidi mafanikio ya EUROPARC yaliopatikana mpaka sasa hivi hapa Ujerumani kama ifuatavyo:
"Kuanzia mwaka 2015 mara moja kwa mwaka hapa Ujerumani tumekuwa na zoezi la shirikisho la washirika wote wa hifadhi chini ya ushirikisho wa pamoja. Ujerumani haijiwakilishi kama wahifadhi wa mbuga tu bali wanajiwakilisha kama wahifadhi wa maeneo aslia ya mazingira. Sisi ni kama mwevuli wa shirikisho hilo. Na kitu hicho ni mafanikio makubwa kwetu, kwa sababu kuna maeneo 137 ambayo yanatokea Ujerumani."
Kwa hivi sasa Ujerumani ina mbuga 17 zenye mimea asilia isiyotumia madawa , na kati ya mbuga hizo 16 zinatambuliwa na Sshirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni ( UNESCO ).
Mbuga 16 za taifa zina eneo jumla la ekari 1.047.859 . Hiyo ni asilimia 0.6 tu ya eneo la nchi nzima .
Mwandishi: Najma Said/BUNDESAMT FÜR NATURSCHUTZ PRESSEMITTEILUNG
Mhariri : Mohamed Abdul- Rahman