1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya Kupambana na Kisukari Duniani

14 Novemba 2018

Leo tarehe 14 Novemba, ni Siku ya kupambana na Kisukari Duniani. Kauli mbiu ya mwaka 2018-2019 ni,‘’ Familia na Kisukari’’

Diabetes-Untersuchung in Südafrika
Picha: picture alliance/Photoshot

Kipindi cha muda miwili kimetolewa kuwa bora katika kufikia kampeni ya Siku ya Kisukari Duniani, kuhusu mpango wa kimkakati wa Shirikisho la Kimataifa la Kisukari na kuwezesha kupanga, kuendeleza, kukuza na kushiriki.

Vifaa na hatua zitakazohukuliwa na shirikisho hilo katika muda huo wa miaka miwili ya kampeni dhidi ya kisukari inapania kutoa hamasisho kuhusu athari ya kisukari kwa familia na mfumo wa kuwasaidia walioathirika. Kadhalika kuzisaidia familia katika juhudi za kukabili, kuwahudumia, kuzuia na kuelimisha kuhusu kisukari.

Picha: Colorbox/M. Anwarul Kabir Choudhury

Zaidi ya watu milioni 425 wameathirika na kisukari. Visa vingi vya ugonjwa huo ni vya daraja ya pili, ambayo inaweza kuzuiwa kupitia mazoezi ya kila siku, vyakula vyenye afya, na kuishi katika mazingira bora. Familia zina jukumu kuu katika kushughulikia mambo yanayichangia kisukari hiyo ya daraja la pili, na lazima wapewe mafunzo, raslimali na mazingira ya kuishi maisha mazuri.

Mtu mmoja kati ya wawili wanaoishi na kisukari bila kutambuliwa. Kugunduliwa mapema na kupata matibabu ni muhimu katika kuzuia matatizo yanayochangiwa na ugonjwa wa kisukari, hivyo uhamasisho kuhusu ishara, dalili, na mambo hatari kuhusu aina zote za kisukari ni muhimu sana ili kusaidia kuugundua mapema.

Sindano ya InsuliniPicha: picture-alliance/dpa/R. Vennenbernd

Ugonjwa wa kisukari unaweza kuwa wa gharama kwa mtu au familia. Katika mataifa mengi, gharama ya sindano ya insulini na ufuatiliaji pekee unaweza kutumia nusu ya mapato familia, na wengi wanashindwa kupata dawa za kisukari mara kwa mara na huduma. Shirikisho la Kimataifa la Kisukari linasema hali hiyo inaashiria kuwa ni lazima kuzuia gharama kuongezwa kwa waathirika na familia zao, suala ambalo linaathiri matokeo ya afya.

Shirikisho hilo linasema kuwa ni mtu mmoja miongoni mwa watu wanne wa familia moja anaweza kufikia mipango ya elimu kuhusu kisukari. Usaidizi wa familia katika kuwahudumia waathiriwa wa kisukari umetajwa kuboresha matokeo ya afya kwa waathiriwa hao.

Kutokana na hilo Shirikisho la Kimataifa la Kisukari limesema ni muhimu kwa elimu inayoendelea kutolewa kuhusu kukabili kisukari kupatikana kwa urahisi kwa waathiriwa pamoja na familia zao, ili kupunguza athari za kihisia ambayo inaweza kuathiri ubora wa maisha.

Mwandishi: Sophia Chinyezi/ www.worlddiabetesday.org

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman