1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya mtoto wa kike yaadhimishwa nchini Tanzania

Veronica Natalis 11 Oktoba 2021

Maadhimisho yanafanyika wakati ambapo mila na desturi pamoja na baadhi ya sheria zinatajwa kuwa ni kikwazo cha kufikia malengo ya watoto wa kike nchini Tanzania.

Südafrika Johannesburg | GirlZ Off Mute
Picha: Thuso Khumalo/DW

Ni kambi inayowahifadhi watoto wa kike waliokimbia katika familia zao wakipinga kulazimishwa kukeketwa na kuolewa. Kambi hii iliyopo Arusha kaskazini mwa Tanzania inawahifadhi mabinti zaidi ya 50 kutoka maeneo mbali mbali ya mikoa ya kanda ya kaskazini hasa kutoka jamii ya wafugaji ya maasai. Mabinti hawa wanapigania ndoto zao baada ya kukatiza masomo kutokana na mila na desturi za makabila yao kuwataka wakeketwe na kuolewa. 

Kero za mashirika ya kiraia

Mashirika ya kiraia nchini Tanzania yanaeleza kuwa marufuku ya wanafunzi wa kike kuendelea na masomo katika mfumo rasmi wa serikali  baada ya kupata ujauzito, bado ni kikwazo cha kufikiwa kwa ndoto za wasichana wengi, kwani wengi wao hukatiza masomo.

Mpaka sasa idadi ya wanafunzi wanaopata ujauzito wakiwa shuleni bado ni kubwa, huku mikoa inayoongoza kwa kuwa na mimba na ndoa za mapema ni Shinyanga, Mwanza, Manyara, Arusha na Katavi.

Soma pia:HRW: Wasichana waliofukuzwa shule kwa sababu ya kupata mimba Tanzania wateseka

Elimu ya afya ya uzazi 

Mpaka sasa idadi ya wanafunzi wanaopata ujauzito wakiwa shuleni bado ni kubwaPicha: Thuso Khumalo/DW

Mradi wa EPIC unaotekelezwa  na Shirika la kimataifa linalohusika na mapambano dhidi ya ukimwi  FHI360 linasema elimu ya afya ya uzazi ni muhimu kuendelea kutolewa kwa vijana ili kuwakinga na madhara ya kiafya yanayokwamisha ndoto zao. Agness Junga ni mwakilishi wa shirika hilo.  

Maadhimisho ya mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu inayosema kuwa kizazi cha kidijitali ni kizazi chetu, ikihamasisha matumizi ya teknolojia ya intaneti kwa vijana kwa ajili ya maendeleo endelevu.