1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya mwisho ya kampeni Ufaransa

5 Julai 2024

Leo ni siku ya mwisho ya kampeni kwa ajlili ya duru ya pili ya uchaguzi nchini Ufaransa, itakayofanyika siku ya Jumapili.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa.
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa.Picha: Aurelien Morissard/Pool/AP Photo/picture alliance

Muungano wa vyama vya mrengo wa kati unaoongozwa na Rais Emmanuel Macron umekubaliana kuachiliana viti na muungano wa mrengo wa kushoto ili kukizuwia chama cha siasa kali za mrengo wa kulia kinachoongozwa na Marine Le Pen kushinda kwenye uchaguzi huo.

Soma zaidi: Vyama vya kihafidhina vyashikilia viti vingi bunge la Ulaya

Ikiwa muungano wa Le Pen utashinda viti 289 kati ya 577 vya bunge, wataweza kuunda serikali itakayoongozwa na mshirika wake, mwenye umri wa miaka 28, Jordan Bardella, kama waziri mkuu.

Ghasia na mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya wagombe na wanasiasa yamekuwa yakiripotiwa, huku wizara ya mambo ya ndani ikisambaza zaidi ya maafisa 30,000 wa polisi kukabiliana na matukio hayo. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW