1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sikukuu ya Eid ul Fitr yanoga, Kenya

10 Aprili 2024

Wakenya wanaadhimisha siku kuu ya Eid ul Fitr wakati ambapo serikali imeitenga kuwa siku ya mapumziko. Sikukuu hii inaadhimishwa wakati bei za bidhaa za matumizi zimeongezeka na gharama za maisha kupanda.

Ethiopia
Waislamu wameswali suala ya Eid, baada ya kumalizika mwezi mtukufu wa RamadhanPicha: Million H.Selase/DW

Jijini Nairobi, baadhi walikusanyika kwenye uwanja wa San Siro Mtaani Majengo, Miskiti wa Jamia na kwengineko. Siku kuu ya Eid ul Fitr inahitimisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan wa siku 30 mfululizo. Mwezi wa Ramadhan ni wa tisa kwenye Kalenda ya kiislamu.

Sherehe hizo huanzia na swala maalum ya Eid Inayofanyika mapema Asubuhi baada ya mwezi mchanga kuonekana. Saa chache zilizopita, Sheikh Abdulhalim Hussein Athman alibainisha kuwa mwezi umeonekana na leo ni siku kuu.

Waislamu washerehekea Eid Ul Fitr, baada ya kumalizika mwezi wa Ramadhani

Mjini Mombasa kwenye uwanja wa Ronald Ngala walikoswali waislamu, Gavana Abdulswamad Sharif Nasir alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kujiepusha na maovu na badala yake kuzingatia maadili.

Wakati huo huo, waziri wa usalama wa Taifa Kithure Kindiki aliitenga rasmi kupitia agizo la gazeti la serikali kuwa siku ya Jumatano ni ya mapumziko kwa sababu ya sherehe za Eid ul Fitr.

Takriban waislamu wote wamesherehekea kwa wakati mmoja

Kina Mama na watoto wao baada ya kuswali suala ya Eid nchini Ethiopia Picha: Million H.Selase/DW

Kwenye kijiji kimoja cha Mkilo kaunti ya Kwale, kwa Mara ya kwanza wamefanikiwa kuswali pamoja na pia kuwapa waislamu mafunzo ya dini katika mwezi mzima wa RAmadhan mtaani kwao na wamefurahia. Abdul Aziz Ali ndio ustadh wa Msikiti wa Masjid Muzdalifa kijijini Mkilo.

Fatuma Abdala Ibrahim ni mkaazi wa Mkilo na anashkuru kuwa wanawake wameungana na kushirikiana Karibu na nyumbani.

Kiongozi mkuu wa Taliban awataka Waafghanistan kuheshimu sharia katika ujumbe wa Eid

Mwezi mtukufu wa Ramadhan huanza Kwa mwezi kuandama na mfungo unaendelea kwa siku 29 au 30 kutegemea utakapoonekana tena mwezi mchanga. Kwa upande Wake Rais William Ruto alituma ujumbe wa kheri njema kwa waislamu wote wanaosherehekea Eid ul Fitr nchini Kenya. Mwanzoni mwa Wiki aliandaa karamu ya Iftar kwenye ikulu ya Nairobi Kabla Ramadhan kukamilika.

Thelma Mwadzaya, DW Nairobi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW