Simba na Yanga kumenyana Jumamosi
18 Oktoba 2024Matangazo
Mchezo maarufu kama Kariakoo Derby utachezwa majira ya saa ya saa kumi na moja jioni kwa saa za Afrika Mashariki katika uwanja wa taifa wa Tanzania, Benjamini Willam Mkapa. Simba ambao ni wenyeji wa mchezo huo watakuwa wanaingia uwanjani na rekodi ya maumivu ambayo kufungwa katika michezo yote ya lihgi ya msimu uliopita na Yanga.
Mpaka sasa Simba wako nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya Tanzania wakiwa na alama 13 baada ya michezo mitano huku Yanga wakiwa nafasi ya nne na alama 12 baada ya michezo minne.
Timu zote mbili Simba na Yanga zipo pia kwenye makundi katika michuano ya shirikisho la soka barani CAF ngazi ya vilabu.