Simba na Yanga wajiandaa kwa robo fainali
25 Machi 2024Mnyama Simba atawakaribisha Al Ahly ijumaa ya Machi 29 huku wananchi Yanga wataumana na Mamelodi Sundowns ya Africa Kusini Jumamosi ya machi 30.
Simba wamekita kambi Visiwani Zanzibar na wachezaji wa simba kuelekea mechi hiyo wanasema "Naamini Timu yangu itatinga nusu Fainali msimu huu kwa sababu Al Ahly tumecheza nao miezi michache iliyopita na tunajua makosa Yao" alisema Golikipa wa Simba Ally Salim.
"Mechi hiyo ni kubwa tunahitaji matokeo naamini uwepo wa Mashabiki uwanjani utatupa nguvu ya kupambana" alisema David Kameta.
Kocha msaidizi wa Simba Seleman Matola anaelezea Hali ya Kambi ya simba kuelekea mchezo huo "Maandalizi kiukweli yapo vizuri sana mechi yetu ipo usiku tumekuwa kifanya mazoezi muda ule ule ambao tunaenda kucheza mechi ni wakati wetu wa kuweka Historia kwa kumvua Bingwa mtetezi na kwenda hatua ya Nusu Fainali kwa sababu tumekuwa tukiishia hatua ya robo fainali”alisema Kocha msaidizi wa Simba Seleman Matola.
Yanga imejipangaje?
Kwa upande wa Yanga ambao watavaana na Mamelodi Sundowns ya Africa Kusini Meneja wa Timu hiyo Walter Harrison anasema "kikubwa ni kuiandaa Timu ili kuweza kuwa katika hali nzuri ya kiushindani kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwadhidi ya Mamelodi Sundowns na tutahakikisha kila kitu kinaenda sawa na furaha kwa wananchi inarejea."
Mechi hizi zinasubiriwa kwa shauku kubwa kuona Simba na Yanga zitafanya nini wachambuzi wa soka wanatazamia hiki "Simba na Al Ahly ni mechi ambayo Al Ahly wanaweza kuingia kwa tahadhari kubwa kuliko mechi zote walizowahi kucheza na Simba kwa sababu wanafahamu katika uwanja wa Benjamin Mkapa Mara mbili mfululizo hawajawahi kupata matokeo ya ushindi mechi zote zitakuwa ngumu kila Timu itakayojiandaa vizuri inaweza kupata matokeo”Alisema Hamis Makila Mchambuzi wa Soka Tanzania.
"Wapizani ambao wanakutana nao na aina ya Madaraja ambayo yapo na mafanikio yanga ananafasi kama atapambana licha ya Yanga kuzidiwa ubora na Mamelodi Sundowns"Alisema Jastin Mhalinga Mchambuzi wa Soka Tanzania
Katika misimu mitano iliyopita, Simba imeingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara tatu huku ikifika hatua hiyo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mara moja na msimu huu wanasaka hatua ya Nusu Fainali.
Mindi Joseph