1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Simba yafufua matumaini ya kutinga robo fainali CAFCL

20 Desemba 2023

Miamba wa soka Wydad Casablanca wako hatarini ya kuondolewa mapema katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kufungwa mabao 2-0 na klabu ya Simba katika uwanja wa Benjamin Mkapa mjini Dar es Salaam.

Kandanda - Ligi ya mabingwa barani Afrika CAF - Simba vs Power Dynamos - Dar es Salaam - Tanzania
Kikosi cha timu ya Simba katika uwanja wa Benjamin Mkapa mjini Dar es SalaamPicha: BackpagePix/empics/picture alliance

Raia wa Cameroon Leandre Onana alifunga mabao mawili ndani ya dakika mbili katika kipindi cha kwanza na kuifanya Wydad Casablanca wa Morocco, mabingwa mara tatu wa michuano hiyo ya CAFCL kupoteza mechi yao ya tatu katika michezo minne iliyocheza ya kundi B.

Ushindi huo wa Simba ni wake wa kwanza kwenye michuano hiyo ya ligi ya mabingwa hatua ya makundi msimu huu.

Soma pia:  Michuano ya African Football League yaanza Tanzania

Wydad Casablanca inaburuta mkia katika kundi B ikiwa na alama 3, nyuma ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast yenye alama 10, Simba ya Tanzaniani ya pili na alama 5 wakati Jwaneng Galaxy ya Botswana imeridhika na alama 4.

ASEC Mimosas imekuwa ya kwanza kufuzu hatua ya robo fainali kwa kuifunga Jwaneng 3-0 mjini Abidjan, wakati vijana wa Belhack Benchikha Simba wamefufua matumaini ya kutinga robo fainali iwapo tu watafanikiwa kupata angalau alama nne katika mechi mbili zilizosalia.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW