SIPRI:Kampuni za silaha zimeongeza faida wakati wa Covid-19
6 Desemba 2021Ripoti ya SIPRI iliyotolewa leo Jumatatu inasema serikali ulimwenguni zimeendelea kununua silaha wakati wa janga la Covid-19, huku baadhi yake zikipitisha hatua za kuyasaidia makampuni ya silaha.
Kwa ujumla makampuni 100 ya juu yameshuhudia ongezeko la faida kwa asilimia 1.3 licha ya uchumi wa dunia kushuka kwa zaidi ya asilimia tatu.
Taasisi ya SIPRI yenye makao yake makuu nchini Sweden, imeongeza kuwa kampuni hizo zimenufaika kutokana na kuingiza fedha taslimu katika uchumi, pamoja na hatua mahususi zilizoundwa kuzisaidia kampuni kama vile malipo ya haraka au mchakato wa kuagiza.
Marekani iliendelea kuongoza katika utengenezaji na mauzo ya silaha duniani, huku watengenezaji wa silaha wa Marekani wakichukua makampuni ya silaha 41 miongoni mwa 100 ya juu duniani. Kati yao, mauzo ya silaha zao ilifikia dola bilioni 285 mnamo 2020 sawa na asilimia 1.9 ya ongezeko ya mwaka hadi mwaka.
China yajidhatiti kijeshi
China ambaye ni mpinzani wa kimkakati, ilikuwa na watengenezaji silaha watano tu miongoni mwa makampuni 100 ya juu duniani, licha ya kasi yake ya kijeshi na uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo. Hata hivyo, mauzo yake ya kila mwaka ya silaha ilikua kwa asilimia 1.5 mwaka jana, ikichukua wastani wa dola bilioni 66.8 katika mauzo mnamo mwaka 2020.
Nan Tian,mtafiti wa kwenye taasisi ya SIPRI amesema katika miaka ya hivi karibuni, makampuni ya silaha ya China yamefaidika na mipango ya kisasa ya kijeshi nchini humo na wamekuwa baadhi ya wanajeshi wa hali ya juu wazalishaji wa teknolojia duniani.
Mauzo ya Urusi yaporomoka
Uingereza, nchi ya tatu kwa uzalishaji wa silaha duniani, ilikuwa na ongezeko ya mauzo ya asilimia 6.2 mnamo mwaka 2020, na kufikia jumla ya dola bilioni 37.5, huku mauzo ya kampuni ya BAE Systems,(kampuni ya silaha ya sita duniani),yakiongezeka kwa asilimia 6.6 pekee. Kwa upande wake Urusi imeshuhudia kupungua kwa mauzo yake ya silaha kwa mwaka wa tatu mfululizo,kutoka dola bilioni 28.2 ya mapato mwaka 2019 hadi dola bilioni 26.4 mnamo 2020, sawa na asilimia 6.5 ya maporomoko.