1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKimataifa

SIPRI: Mapato ya silaha duniani kwa mwaka 2023 yaliongezeka

Angela Mdungu
2 Desemba 2024

Taasisi ya kimataifa ya masuala ya Amani SIPRI imebainisha kuwa kampuni 100 za silaha kubwa zaidi duniani zilishuhudia ongezeko la mauzo ya silaha mwaka uliopita na kufikia zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 600.

F-35
Ndege ya kivita ya ya kivita ya Marekani Lockheed Martin F-35Picha: picture alliance/dpa/dpa-Zentralbild

Ongezeko hilo lilichochewa na mizozo ya Ukraine, Gaza pamoja na mivutano mikubwa ulimwenguni. Kwa mujibu wa ripoti ya taasisi hiyo ya mjini Stockholm, mapato ya kampuni 100 za silaha yaliongezeka kwa asilimia 4.2 sawa na dola za Kimarekani bilioni 632.

Mapato ya silaha yanajumuisha mapato yanayotokana na mauzo ya bidhaa za kijeshi  na huduma kwa wateja wa jeshi kitaifa na kimataifa. Taasisi ya SIPRI imebainisha kuwa kampuni nyingi za silaha ziliongeza utengenezaji wa bidhaa hizo na kubashiri kuwa ongezeko la mauzo huenda likaendelea.

Ripori hiyo imeeleza kuwa makampuni ya Marekani yalichangia karibu nusu ya mapato ya silaha kote duniani ambayo ni ongezeko la asilimia 2.5 sawa na dola za Kimarekani 317.

Taasisi hiyo ya kimataifa ya masuala ya amani  imesema kampuni kubwa zaidi za silaha duniani, Lockheed Martin na RTX hata hivyo yaliporomoka kidogo kimapato. Imeeleza kuwa kwa ujumla kampuni ndogo za kutengeneza silaha zilikuwa na ufanisi zaidi katika kukidhi mahitaji yaliyotokana na vita vya Ukraine na Gaza, sambamba na mivutano ya Asia Mashariki.

Kampuni ya silaha ya Urusi ilipata ongezeko kubwa la mapato

Taasisi hiyo ilibaini kukua kwa kasi kwa kampuni za silaha za Urusi na Mashariki ya kati. Kampuni inayomilikiwa na serikali ya Urusi ya Rostec inayozidhibiti kampuni nyingine kadhaa za ulinzi za nchi hiyo ilipanda kwa mauzo na kufikia nafasi ya saba ikiwa na ongezeko la mauzo la asilimia 49 na kupata bilioni 21.7.

Kombora jipya aina ya Sarmat lililotengenezwa UrusiPicha: picture-alliance/AP Photo/Russian Television

Mapato ya mauzo ya silaha zake yalikuwa juu mara kumi zaidi ya kampuni pekee ya Ukraine iliyoorodheshwa ya JSC iliyopata dola bilioni 2.2 baada ya ongezeko la asilimia 69.  SIPRI inaarifu kuwa hata hivyo taarifa kuhusu utengenezaji wa silaha nchini Urusi ni kidogo na ni za kutiliwa shaka.

Soma zaidi:Mauzo ya silaha Ulaya yaongezeka kwa vita vya Ukraine

Kampuni sita za Mashariki ya katika 100 zenye mauzo makubwa ya silaha zinajumuisha kampuni tatu za Israel, tatu za Uturuki na kwa ujumla ziimechangia mauzo ya silaha kwa asilimia 18 kutokana na vita vya Gaza na Ukraine. Kwa upande wa Ulaya ukiachilia mbali Urusi, mauzo ya silaha yalikuwa kidogo kuliko eneo lolote duniani.

Mauzo hayo yaliongezeka kwa asilimia 0.2 sawa na dola bilioni 133.  Sababu ya mauzo kidogo Ulaya ni kuwa kampuni barani humo zilikuwa zikifanyia kazi mikataba ya zamani inayohusu mifumo migumu ya silaha hivyo takwimu hazikuakisi ongezeko katika silaha zilizoagizwa baada ya mapitio ya mikataba.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW