1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKimataifa

SIPRI: Vichwa vya nyuklia vinawekwa katika hali ya tahadhari

17 Juni 2024

Taasisi ya kimataifa ya utafiti wa masuala ya amani na usalama SIPRI imesema leo kuwa mataifa yenye silaha za nyuklia yanaimarisha uwezo wa silaha zao za nyuklia katika muktadha wa migogoro inayoendelea duniani kote.

Urusi | Wanajeshi wa Urusi wanapakia kombora la Iskander kama sehemu ya luteka za kijeshi katika eneo lisilojulikana nchini Urusi.
Wanajeshi wa Urusi wanapakia kombora la Iskander kama sehemu ya luteka za kijeshi katika eneo lisilojulikana nchini Urusi.Picha: Russian Defense Ministry Press Service/AP Photo/picture alliance

Kulingana na ripoti mpya iliyochapishwa na taasisi ya SIPRI, idadi ya vichwa vya nyuklia vilivyowekwa katika hali ya tahadhari inaongezeka kwa kasi.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo ya kimataifa ya utafiti wa masuala ya amani na usalama Dan Smith ameeleza kuwa ongezeko la idadi ya vichwa vya nyuklia kunatia wasiwasi.

Soma pia: SIPRI: Matumizi ya kijeshi yaongezeka duniani

Kadhalika, ripoti hiyo imesema idadi ya maendeleo ya silaha za nyuklia pia imeongezeka huku mataifa yenye nguvu za silaha za nyuklia zikionekana kutumia nadharia ya kuyatisha mataifa mengine kutotumia silaha zao za nyuklia la sivyo huenda zitashambuliwa iwapo zitafanya hivyo.

Korea Kaskazini ni miongoni mwa nchi zenye silaha za nyuklia

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akilihutubia bunge la nchi hiyoPicha: KCNA/REUTERS

Kati ya jumla ya vichwa vya nyuklia 12,121 vilivyoorodeshwa duniani kote mnamo mwezi Januari, karibu 9,585 vilikuwa sehemu ya hifadhi ya kijeshi kwa ajili ya kutumika.

Takriban vichwa 3,904 vya nyuklia tayari vimeungansihwa kwenye makombora na ndege za kivita - idadi hiyo ikiwa 60 zaidi tofauti na mwezi kama huo mwaka uliopita. Kulingana na ripoti hiyo, vichwa vilivyobaki vimehifadhiwa.

Kwa miongo kadhaa, idadi ya silaha za nyuklia duniani kote imekuwa ikipungua tangu kumalizika kwa vita baridi. Hata hivyo, licha ya kupunguza hifadhi zake za nyuklia, Marekani na Urusi bado zinamiliki idadi kubwa ya silaha zote za nyuklia duniani.

Kulingana na SIPRI, nchi tisa zina silaha za nyuklia: kando na Urusi na Marekani, zipo pia China, Ufaransa, Uingereza, Pakistan, India, Israel na Korea Kaskazini.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW