1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SIRTE Afrika yataka viti vya kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa

6 Julai 2005

Viongozi wa umoja wa Afrika wamepitisha azimio la pamoja wakitaka viti viwili vya kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa. Katika mkutano wao mjini Sirte nchini Libya, viongozi hao wamesema lengo lao ni kuvitumia viti hivyo kuwa na kura ya turufu. Hata hivyo hawakusema vipi wajumbe wa umoja huo watakavyochaguliwa, lakini Misri, Afrika Kusini na Nigeria zina nafasi nzuri ya kuliwakilisha bara la Afrika katika baraza hilo.

Hapo awali, muandalizi wa mkutano huo, rais Muammmar Gaddafi, wa Libya, alisema Afrika lazima ikome kuomba misaada na badala yake kujikakamua kuyatanzua matatizo yake yenyewe. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan aliuambia mkutano huo ana matumaini makubwa kwamba viongozi wa mataifa ya G8 watazungumzia usawa wa biashara kama njia ya kupunguza umaskini barani Afrika wakati wa mkutano wao huko nchini Scotland.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW