1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Slovakia yatishia kuchukua hatua dhidi ya wakimbi wa Ukraine

Sylvia Mwehozi
3 Januari 2025

Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico aliyekasirishwa na hatua ya Kiev ya kusimamisha mkataba wa usambazaji gesi ya Urusi, ametishia kuchukua hatua dhidi ya wakimbizi wa Ukraine.

Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico
Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico Picha: Artyom Geodakyan/TASS/IMAGO

Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico aliyekasirishwa na hatua ya Kiev ya kusimamisha mkataba wa usambazaji gesi ya Urusi, ametishia kuchukua hatua dhidi ya wakimbizi wa Ukraine.

Akizungumza katika mji mkuu wa Bratislava, Fico alisema kuwa atajadiliana na muungano wa serikali yake juu ya uwezekano wa kupunguza uungwaji mkono kwa wakimbizi wa Ukraine walioko nchini mwake. Waziri huyo mkuu pia amerudia kitisho chake kwamba Slovakia inaweza kusimamisha usambazaji wa umeme kwa nchi jirani ya Ukraine.

Ukraine iliyoharibiwa na vita, ilisimamisha mkataba wake na kampuni kubwa ya nishati ya Urusi Gazprom kwa usafirishaji wa gesi ya Urusi kuelekea nchi za magharibi kupitia nchi hiyo.

Slovakia ni miongoni mwa nchi zilizoathirika, ingawa nchi nyingine nyingi za Umoja wa Ulaya zimejiandaa kwa hatua hiyo iliyotangazwa kwa muda mrefu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW