1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Slovenia mabingwa wa Ulaya

Sekione Kitojo
18 Septemba 2017

Slovenia kwa mara ya kwanza imetawazwa mabingwa wa mchezo wa kikapu barani Ulaya

Türkei FIBA EuroBasket 2017 Slowenien - Serbien
Wachezaji wa Slovenia wakisherehekea ubingwa wa Ulaya wa Basket ballPicha: picture-alliance/abaca/A. Dumanli

Slovenia  imesherekea  ushindi  wa  kwanza  wa  taji  la  ubingwa wa  Ulaya  katika  mchezo  wa  mpira  wa  kikapu , basket ball  kwa mwaka  2017  baada  ya  kuishinda  Serbia  katika  fainali  ya mashindano  hayo  barani  Ulaya  jana  Jumapili . Slovenia  ilifikia nusu  fainali  katika  michezo  hiyo  mwaka  2009 lakini  ilimaliza  kwa kushika  nafasi  ya  nne.

Wachezaji wa Serbia wenye jezi nyekundi wakijaribu kumzuwia mchezaji wa Slovenia kufungaPicha: picture-alliance/AP Photo/E. Gurel

Serbia  iliishinda  Finland katika  awamu  ya  makundi  mjini  Helsinki na  pia  kuzishinda   Ugiriki  na  Ufaransa   katika  kundi  lao. Katika awamu  ya  mtoano  Slovenia  iliishinda  Ukraine na  pia  Latvia  na kuingia  katika  robo  fainali. Waliwashangaza  wengi  walipofanikiwa kuwashinda  mabingwa  watetezi Uhispania  katika  nusu  fainali. Na katika  fainali  Slovenia  ilikuwa  inasubiriwa  na  Serbia  iliyofikia fainali  za  kombe  la  dunia  la  mpira  wa  kikapu  mwaka  2014  na 2016 na  kushindwa  katika  fainali  hizo  na  Marekani. lakini hatimaye Slovenia  ilitoka  kidedea  kwa  ushindi  dhidi  ya  Serbia .

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / dpae / ape / rtre / afpe

Mhariri: Yusuf , Saumu