1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Slovenia yapiga marufuku safari za Netanyahu

25 Septemba 2025

Serikali ya Slovenia imepiga marufuku Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuingia nchini humo, hatua inayochochea zaidi mivutano ya kidiplomasia kati ya Ljubljana na Tel Aviv.

Ujerumani Berlin 2015 | Mapokezi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Angela Merkel.
Waziri wa Mambo ya nje wa Slovenia Neva Grasic amesema Netanyahu ana kesi nyingi zinazomkabili na hivyo hawezi kukanya nchini humo.Picha: Christian Thiel/IMAGO

Serikali ya nchi hiyo ya Ulaya ilitangaza Alhamisi kuwa marufuku hiyo inakuja baada ya Slovenia kutambua rasmi taifa la Palestina mwaka jana na kuchukua hatua kali dhidi ya mawaziri wawili wa mrengo mkali wa kulia wa Israel mwezi Julai.

Neva Grasic, Waziri wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje, alisema kupitia ukurasa wa serikali kwenye X kwamba hatua hiyo ni uthibitisho wa kujitolea kwa Slovenia kutetea sheria za kimataifa na haki za binadamu.

Slovenia, ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya, pia iliweka vikwazo vya silaha dhidi ya Israel mwezi Agosti na kupiga marufuku uagizaji wa bidhaa zinazozalishwa katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu.

Grasic aliongeza kuwa serikali imechukua hatua hiyo kwa sababu Netanyahu anakabiliwa na mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu uhalifu wa kivita unaodaiwa kufanywa Gaza.

Wakati Slovenia ikichukua hatua ya kumpiga marufuku Netanyahu, viongozi kama Viktor Orban wa Hungary wanazidi kumkumbatia na kumpokea.Picha: Attila Kisbenedek/AFP/Getty Images

Msimamo wa wazi wa Slovenia

"Umma unafahamu kwamba kesi zinaendelea dhidi yake kwa tuhuma za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu,” alisema Grasic, akibainisha kuwa Slovenia inatuma ujumbe wazi kwa Israel kuhusu umuhimu wa kuheshimu maamuzi ya mahakama za kimataifa na sheria za kibinadamu.

Kwa muda mrefu, nchi hiyo ndogo ya milima ya Alpine imekuwa miongoni mwa sauti zinazotaka kusitishwa kwa mapigano Gaza na kuongezwa kwa misaada ya kibinadamu kwenye ukanda huo.

Mwezi Julai, Slovenia iliweka marufuku ya usafirishaji na uagizaji wa silaha kwenda na kutoka Israel, hatua iliyofuata baada ya mawaziri Itamar Ben-Gvir na Bezalel Smotrich kutangazwa kutotakiwa nchini humo kutokana na kauli za "kuchochea mauaji ya halaiki” dhidi ya Wapalestina.

Aidha, mwezi Agosti Slovenia iliendeleza msimamo wake kwa kupiga marufuku bidhaa kutoka maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na kupitisha kifurushi kipya cha misaada kwa wakazi wa Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW