1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SMS zinapotumika kuokoa maisha Ghana

7 Septemba 2012

Wakati mji wa Accra ukishuhudia matukio mengi ya ujambazi wa kutumia silaha, Herman Chinery-Hesse amebuni mfumo wa tahadhari unaotumia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi kuwalinda raia kutokana na mashambulizi hayo.

Mvumbuzi wa huduma ya "Hei Julor", Herman Chinery-Hesse wa Ghana.
Mvumbuzi wa huduma ya "Hei Julor", Herman Chinery-Hesse wa Ghana.Picha: Lindy Larson

Mvumbuzi wa programu hii ya Kighana Herman Chinery-Hesse alitaka kuchukua hatua dhidi ya matukio ya ujambazi wa kutumia silaha mjini Accra. Ndivyo alivyokuja na programu hii ya "Hei Julor" au "Ewe mwizi" kwa lugha ya wenyeji wa mji huo.

"Hei Julor" ni programu ya mfumo wa usalama inayotumiwa katika simu ambapo mtu anaweza kutuma ujumbe mtupu kutoka kwenye simu zaidi ya tano zilizosajiliwa katika eneo, pale makaazi ya mtu au biashara yanapovamiwa.

Hatua hii inasababisha kutumwa kikosi cha waokoaji kutoka kampuni binafsi ya ulinzi, na wakati huo huo watu wengine kumi wakiwemo majirani na marafiki wanapata ujumbe huo na wanaweza kufika haraka nyumbani kwa mhusika ili kumsaidia.

Huduma hii ya Hei Julor ilizinduliwa chini ya mwaka moja nyuma, wakati wa vuguvugu la mageuzi katika mataifa ya kiarabu na wakati ambapo maandamano ya vrugu yalikuwa yanafanyika nchini Uingereza.

Chinery-Hesse: "Baba wa Teknolojia Afrika"

Katika matukio yote mawili, teknolojia ya simu za mkononi kama vile ujumbe wa Blackberry au BBM ulikuwa ukitumika kuratibu shughuli. Chinery-hesse, ambaye amepewa jina la baba wa teknolojia barani Afrika anakumbuka jinsi yeye na marafiki zake walivyokuja na wazo la "Hei Julor."

Herman Chinery-Hesse akiwa ofisini wake.Picha: Isaac Kaledzi

"Tulikuwa tunafuatilia maandamano katika nchi za kiarabu and nchini Uingereza kupitia redio mchana moja na ikatujia akilini kuwa walikuwa wakitumia BBM kuratibu maandamano hayo. laazima itakuwa na manufaa makubwa kwa jamii yetu, katika utamaduni wetu au nchi yetu. Na kwa sababu hiyo, tulikuja na wazo la "Hei Julor."

Haikuwachukulia muda Chinery-Hesse na marafiki zake wanaofanya kazi katika kampuni ya programu za kompyuta ya "Softribe" kuweka mawazo hayo katika vitendo.

"Tumekuwa wataalamu kwa vile hii ndiyo kazi tunayoifanya kazini kwetu, kwa hiyo tulikuwa na vifa vyote vinavyohitajika. Tulikaa ofisini, tukamualika kila moja kuhudhuria kikao na kujadili namna ya kuja na huduma ambayo kila moja angeweza kuipata kwa bei nafuu na kuizuia Ghana kuwa taifa la wahalifu." Anasema Chinery-Hesse.

Namna ya Kutumia "Hei Julor"

Ili kujiunga na huduma hii mteja anahitaji kununua kadi yenye kodi, ambayo mteja anaituma kwa kampuni hiyo. Chinery-Hesse anasema programu hiyo imesanifiwa kwa ajili ya wenye uwezo mkubwa na hata waliyo na uwezo mdogo. Anasem wateja wenye uwezo mkubwa wanaweza kulipia huduma hiyo kwa mwaka mzima, na wale wenye uwezo mdogo wanalipa cedi 10, sawa na euro 4 kwa mwezi.

Wafanyakazi wawili wa huduma ya Hei Julor nchini Ghana.Picha: Isaac Kaledzi

Teknolojia hiyo imeokoa maisha ya baadhi ya watu. Chinery-Hesse anakumbuka mifano ya watu wawili hivi karibuni.

"Wa kwanza alikuwa mwanaume moja mzee aliyepatwa na kiharusi na kulikwepo na watu nyumbani kwake lakini yeye alikuwa ghorofa ya juu na alikosa nguvu za kushuka chini au kupiga ukelele wa kuomba msaada lakini simu yake alikuwa nayo kwa hiyo alichokifanya na kutuma Hei Julor mchana, na kampuni ya ulinzi ilikuja kumpeleka hospitali."

Kituo cha mawasiliano cha kampuni hiyo ni kodogo sana lakini kikiwa na vyombo vya kuhefadhi na kusambaza taarifa za intanet duniani kote. Kwa mujibu wa afisa moja wa juu, wafanyakazi mar nyingi huwa na kompyuta aina ya laptop ili kuwa na mawasiliano na wateja wakati wote. Mkurugenzi wa kampuni ya Softribe, Anthonio Tettey anasema kwa sasa wana wateja zaidi ya alfu moja.

Mwandishi: Kaledzi Isaac/ Iddi Ismail Ssessanga
Mhariri: Sekione Kitojo

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW