Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu elimu, Sayansi na Teknolojia UNESCO inakadiria kuwa mmoja kati ya wasichana kumi Kusini mwa jangwa la Sahara hukosa kuenda shule wanapopata hedhi kwa sababu ya kukosa sodo. Msanii wa Uganda Sadat Nduhira amekuwa akiwafundisha wasichana namna ya kujitengenezea sodo kwa njia rahisi.