1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sofia. Bulgaria inafanya uchaguzi mkuu.

25 Juni 2005

Uchaguzi mkuu unaendelea hivi sasa nchini Bulgaria. Kura ya maoni inaonesha kuwa chama cha Kisoshalist, kilichoundwa kutokana na chama cha zamani cha Kikomunist mwaka 1990, kinaongoza kwa kiasi cha asilimia 15 mbele ya chama cha waziri mkuu Simeon Sax-Coburg cha mrengo wa kati kulia.

Wachunguzi wanasema kuwa vyama zaidi ya saba vinaweza kuingiza wabunge katika bunge la nchi hiyo, na kwamba Wasoshalist watahitaji kuungana na vyama vingine ili kuweza kuunda serikali mpya.

Katika wakati wa kampeni , Wasoshalist waliahidi kuyaondoa majeshi ya Bulgaria kutoka nchini Iraq pamoja na kuboresha huduma za jamii.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW