1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SOFIA-Bunge la Bulgaria laafiki mkataba wa kujiunga na Umoja wa Ulaya

11 Mei 2005

Bunge la Bulgaria leo limeidhinisha kwa kauli moja mkataba wa kujiunga na Umoja wa Ulaya na hivyo kujiweka katika uwezekano mkubwa wa kuingia katika Umoja huo itakapofika mwaka 2007.

Kati ya Wabunge 234 waliopiga kura,watatu tu ndio walipiga kura ya kupinga.

Bulgaria inatazamia kupatiwa msaada wa Mabilioni ya Euro mara itakapojiunga na Umoja wa Ulaya.

Hata hivyo kwanza inalazimika kufanyia mageuzi masuala makuu kadhaa,yakiwemo ya kuweka hali bora ya mfumo wa sheria na kuepuka vitendo vyovyote vitakavyovuruga hali ya usalama,ambavyo huenda vikaichelewesha nchi hiyo kukubaliwa ndani ya Umoja huo kwa mwaka mzima.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW