Soka. Bayern yaonja kipigo.
11 Novemba 2007Matangazo
Katika ligi ya soka ya Ujerumani mabingwa watetezi VFB Stuttgart wamewashindwa Bayern Munich kwa jumla ya mabao 3-1. Hiki ni kipigo cha kwanza kwa Bayern katika msimu huu wa Bundesliga, lakini wamebaki wakiongoza ligi hiyo licha ya kipigo hicho . Katika michezo mingine ya Bundesliga Rostock iliishinda Energy Cottbus kwa mabao 3-2, Hertha BSC Berlin ikaishinda Hanover kwa bao 1-0, Werder Bremen ikaizamisha Karlsruhe kwa mabao 4-0, Schalke 04 ikatoka sare ya bao 1-1 na Hamburg SV na Borussia Dortmund nayo ikatoka sare pia ya bao 1-1 na Eintracht Frankfurt.