Soka: Klabu zilizotinga 16 bora ya Champions League
26 Februari 2026
Siku ya Jumanne na Jumatano zilishuhudiwa mechi za mchujo kwa timu ambazo hazikufanikiwa kufuzu moja kwa moja katika hatua hiyo ya ligi ya mabingwa.
Mabingwa wa mara nyingi wa michuano hiyo Real Madrid waliendeleza ubabe wao kwa Benfica ya Ureno kwa kuwacharaza 2-1 katika mechi ya marudiano na kusonga mbele hatua ya 16 bora.
Mechi ya awali iliyokubwa na misukosuko kwa tukio la nyota wa Real Madrid, Vinicius Jr kudai kufanyiwa vitendo vya ubaguzi na mchezaji wa Benfica, Madrid alishinda 1-0.
PSG ya Ufaransa ambayo ndiyo mabingwa watetezi nayo ilifanikiwa kufuzu japo kwa mbinde baada ya sare ya 2-2 dhidi ya majirani zao Monaco. Sare hiyo imeifanya PSG kusonga mbele kwa jumla ya magholi 5-4.
Borussia Dortmund ya Ujerumani imetupwa nje ya michuano hiyo baada ya kuambulia kichapo cha magoli 4-1 dhidi ya Atalanta ya Italia.
BVB walishinda mchezo wa kwanza 2-0 mjini Dortmund dhidi ya waitaliano hao lakini waliposafiri kwenda Italia waliangua pua.
Droo ya Robo fainali kufanyika Ijumaa
Jumla ya timu 16 zinaisubiria kwa hamu droo ya mechi zao zijazo itakayofanyika Ijumaa nchini Uswisi.
Timu hizo ni Arsenal, Bayern München, Liverpool,Tottenham, Barcelona, Chelsea, Sporting CP, Man City, Real Madrid, PSG, Newcastle, Atletitico Madrid, Atalanta, Leverkusen, Galatasaray, na Bodø/Glimt.
Fainali ya UEFA msimu huu itachezwa mjini Budapest, Hungary tarehe 30, Mei.